WEWE NI MUNGU
by Florence Mureithi
Vizazi hadi Vizazi, Vya kufahamu wewe
Uliye Mungu wa kale na uliye Mungu wa leo
Kazi zako zaonyesha ukuu wako wewe
Umetukuka umeinuliwa ewe bwana
Kweli wewe wewe ni Mungu
Kweli wewe wastahili
Umeketi juu sana, kwenye kiti cha enzi
Umejivika utukufu, wewe ni Mungu
Nikitazama matendo yako na nguvu zako wewe
Yadhihirika machoni mwangu wengine wote ni miungu
Uumbaji wako waonyesha hekima yako wewe
Watukuzwa kati ya mataifa milele bwana