Kijito Cha Utakaso
by Beatrice
Kijito cha utakaso ni damu ya Yesu
Bwana anao uwezo kunipa wokovu
Viumbe vipya naona, Damu ina nguvu
Imeharibu uovu, uliyo dhulumu
Kijito cha utakaso
Nizame kuoshwa humo
Namsifu Bwana kwa hiyo
Nimepata utakaso
Naondoka kutembea, nuruni mwa mbingu
Na moyo safi kabisa kumpendeza Mungu
Ni neema ya ajabu kupakwa na damu
Na Bwana Yesu kujua Yesu wa msalaba