Baba Yetu

by Ruben Kagame

Baba yetu wa mbinguni tunaleta sifa kwako Wewe hulinganishwi na yeyote duniani Mbingu na nchi zakusifu, jua na mwezi vyakutukuza Wanyama wa pori, ndege wa angani Sifa tele kwako Bwana Hoiye! Sifa zetu, Hoiye! ni zako zote Hoiye! Usifiwe, Hoiye! Milele Bwana Tukiomba kwako Baba, sikio lako li wazi kwetu Macho yako yatuona; sisi watoto wako Ulimtoa Yesu, mwana wako wa pekee Alikufa msalabani; sasa tuko huru